Uwekezaji Wa Pamoja
Mipango ya uwekezaji wa pamoja ni mojawapo ya taasisi za masoko ya mitaji. Vyombo hivi hutakiwa kuteua wadhamini na meneja ambaye atasimamia mfuko. Wataalam hawa wataingia kwenye mkataba wa usimamizi wa mfuko huu na kuteua wataalamu wengine kama wakaguzi wa hesabu, wanasheria na wauzaji wa vipande na wapokeaji wa fedha na msajili. Utaratibu huu huwezesha kukusanya mitaji na kuiwekeza kwenye miradi mbalimbali mtawanyo. Mfano wa taasisi za uwekezaji wa pamoja hapa Tanzania ni pamoja na Mfuko wa Umoja, kampuni ya NICOL na ile ya chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda (TCCIA Investment Limited); vile vile Mfuko wa Wekeza Maisha, Jikimu na Mfuko wa Watoto.
Utaratibu wa Kuanzisha Mipango ya Uwekezaji wa Pamoja:
Mfuko wa Dhamana (Unit Trust)
Utaratibu wa kuanzisha mfuko wa dhamana ni kama ifuatavyo:
- Meneja na mdhamini wanatakiwa kuleta maombi ya kuidhinisha mpango wa uwekezaji wa pamoja Mamlaka;
- Baada ya kibali kutolewa kwa meneja na mdhamini, wahusika hawa hutakiwa kuwasilisha makabrasha yafuatayo kwa Mamlaka ili kupata idhini ya kuanzisha mfuko wa dhamana:
- Kukamilisha fomu ya maombi
- Mipango inayoainisha utaratibu wa kualika umma kununua vipande vya mfuko wa dhamana
- Kuwasilisha ripoti ya mahesabu ya Mdhamini iliyokaguliwa;
- Barua ya kukubali kuwa mdhamini inatakiwa kuwasilishwa Mamlaka;
- Makubaliano ya mfuko;
- Mikataba mingine yoyote inayohusu mfuko;
- Katiba ya kampuni inayosimamia mfuko;
- Majina ya wadhamini;
- Majina ya meneja wa mfuko;
- Majina ya washauri wa uwekezaji wenye uzoefu wa kuanzisha na kuendeleza mipango ya uwekezaji wa pamoja;
- Majina ya washiriki wengine kwenye mipango ya uwekezaji wa pamoja wenye uzoefu na uadilifu wa hali ya juu;
- Nyaraka nyinginezo zinazohusu mfuko;
- Malipo ya kuomba kuandikishwa mfuko.
Kampuni za Uwekezaji
Utaratibu wa kuanzisha kampuni ya uwekezaji wa pamoja ni kama ifuatavyo:
- Meneja na mdhamini wanatakiwa kuwasilisha maombi ya kuwa wasimamizi wa kampuni kwenye ofisi za mamlaka;
- Wakishapewa kibali, watatakiwa kuwasilisha maombi ya kuidhinisha mfuko ya kiambatanishwa na:
- Fomu ya maombi;
- Katiba na kanuni za kampuni inayojumuisha maelezo kuhusu utaratibu wa kualika umma kununua hisa
- Waraka wa toleo wenye maelezo yote kuhusu hisa zinazotolewa;
- Mahesabu ya mdhamini yaliyokaguliwa;
- Barua kutoka kwa mdhamini ikikubali kuteuliwa kuwa Mdhamini;
- Mikataba yoyote inayohusu kampuni ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na makubaliano na mikataba ya kazi;
- Katiba ya kampuni itakayoongoza kampuni hii ya uwekezaji (inaweza kuwa ya jaribio kama kampuni haijasajiliwa);
- Majina ya meneja;
- Majina ya washauri wa uwekezaji ili kuridhisha Mamlaka ya kuwa washauri wana uzoefu, ni waaminifu na wenye kufuata maadili. Nakala ya makubaliano ya ushauri wa uwekezaji inabidi iwasilishwe kwa Mamlaka;
- Majina ya wadhamini ili kuridhisha Mamlaka ya kuwa mdhamini ana uzoefu, ni mwaminifu na mwenye kufuata maadili. Nakala ya makubaliano ya udhamini inabidi iwasilishwe kwa Mamlaka;
- Majina mengine ya wadau wanaohusika na kampuni ya uwekezaji ili kuridhisha Mamlaka ya kuwa wahusika wana uzoefu, na ni waminifu;
- Nyaraka nyinginezo kama zitakavyotakiwa na mamlaka
- Malipo ya kuandikisha kampuni.