Namna ya Kufanya Maombi

Uwasilishaji wa maombi

Maombi yawasilishwe kwa Mamlaka kwa kupitia tovuti ya Mamlaka au uwasilishaji wa maombi ufanyike kwa kupeleka barua, fomu (ambayo imeambatanishwa katika kipengele cha leseni katika tovuti hii) na viambatanisho kwa Mamlaka. Tafadhali elewa kwamba malipo yanatakiwa yalipwe mwanzoni au yaambatanishwe pamoja na maombi ya leseni kwa njia ya hundi ya kampuni au amana ya kuingiza fedha benki (deposit slip).

Nyaraka za uhakiki wa vigezo

Mamlaka inatakiwa kuhakikisha kwamba kila mtu ambaye ni mkurugenzi, mtendaji mkuu, meneja, msimamizi wa watu muhimu wenye leseni wamehakikiwa na kuonekana wanavigezo stahiki vya kushikilia nyadhifa hizo walizonazo. Katika kuhakikisha kwamba wakurugenzi, mtendaji mkuu, meneja na watu muhimu wanaoomba leseni wana vigezo stahiki, Mamlaka inataka waombaji wa leseni kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

  • Kivuli cha nyaraka ya kitambulisho cha taifa/hati ya kusafiria iliyohakikiwa;
  • Wasifu uliojitosheleza wa wakurugezi au mtu muhimu (kama ilivyoainishwa katika jedwali la kwanza, Kanuni 1 (h) ya kanuni za leseni, Chapisho la Serikali Namba 417 ya mwaka 1996;
  • Kivuli cha nyaraka cha uhakiki wa Jeshi la polisi kutoka katika kitengo cha kupepeleza mambo ya jinai (au kinachoshahibiana kutoka nchi za nje);Kujaza fomu ya uhakiki wa vigezo. Pakua