Uchunguzi

Moja ya kazi za msingi za Mamlaka ni kukuza na kudumisha kiwango cha juu cha uaminifu katika soko kwa maslahi ya washiriki wa soko na Umma. Mamlaka pia inalazimika chini ya kifungu cha 10 cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, 1994:

  • kufanya mambo yote muhimu ili kuhakikisha kwamba soko lake lina usawa na haki kwa washiriki;
  • kuwa na uwezo wa kutosha kuchunguza malalamiko ya wawekezaji kuhusiana na shughuli za uwekezaji kwenye soko; na
  • kuwa na mipango ya kutosha ya ufuatiliaji, uchunguzi na kuhakikisha Sheria, Kanuni na Miongozo katika soko inafuatwa.

Uchunguzi hufanywa na Kurugenzi ya Sheria na Utekelezaji kwa kushirikiana na Kurugenzi ya Usimamizi wa Masoko. Uchunguzi hufanywa kwa njia ya mahojiano, kuchunguza nyaraka na mifumo ya kampuni.