News

Posted On: Sep, 01 2020

TAHADHARI UPATU HARAMU

News Images

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) inapenda kutahadharisha Umma kuwa kuna matangazo ya uwepo wa fursa za uwekezaji danganyifu kupitia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Facebook, Twitter na Instagram zikishawishi Umma kuwekeza katika kampuni na mipango ya uwekezaji wakiahidiwa kupata faida ya asilimia 150% kila siku na kutoa gawio la faida kila baada ya siku 3 kwa kuwekeza kwenye biashara hizo. CMSA inatahadharisha Umma kuwa mipango hiyo ni upatu haramu (pyramid schemes) na wananchi wako katika hatari ya kupoteza fedha zao. Taarifa zaidi pakua hapa >>> tangazo la umma upatu haramu